Katibu Tawala Wilaya ya Chamwino Ndg. Neema Nyalege ahimiza mashirikia yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) kutoa taarifa zao za utekelezaji wa shughuli wanazozifanya ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kila mwaka kama sheria inavyoelekeza
Hayo ameyasema leo Juni 20, 2025 wakati akimuwakilisha Mkuu wa Wilaya ya Chamwino Mhe. Janeth Mayanja katika Jukwaa la mwaka 2025 la mashirika yasiyo ya Kiserikali (NGO’s) lililofanyika katika ukumbi wa mikutano wa Halmashauri ambalo hufanyika kila mwaka kwa kuwakutanisha wadau pamoja na mashirika yasiyo ya kiserikali yanayotekeleza miradi mbalimbali ya maendeleo na kutoa huduma kwa jamii ndani ya Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Ndg. Neema Nyalege ameyasema hayo kufuatia baadhi ya mashirika kutowasilisha taarifa zao za utandaji wa kazi wanazozifanya pamoja na taarifa za fedha ambazo hutakiwa kwa mujibu wa sheria kuwasilishwa kwa Serikali, na hivyo kuelekeza kuchukuliwa kwa hatua kwa mashirika yasiyo wasilisha taarifa hizo kulingana na adhabu (faini) kama zilivyohainishwa.
Aidha, ametoa rai kwa mashirika hayo yasiyo ya kiserikali kuhakikisha wanafanya kazi kwa uwazi na uwajibikaji wakati wanatekeleza majukumu yao katika ngazi mbalimbali kuanzia ngazi ya Halmashauri, Kata hadi Kijiji ili kutokuleta migongano.
Halikadhalika Bi. Nyalege amehimiza pia mashirika hayo kuhakikisha wanakamilisha ulipaji wa ada zao za kila mwaka ambazo hulipwa kwa Serikali ili kuhakikisha sekta hiyo inasonga mbele kwa manufaa ya wengi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.