Mafunzo ya siku tatu yameendeshwa na Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino, kwa walimu wa shule za msingi hapa wilayani kuhusu ‘mabadiliko ya tabianchi’.
Mafunzo hayo yaliyohitimishwa leo Februari 14, 2026 yamejumuisha mada mbalimbali za kujenga uelewa kuhusu mabadiliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na vyanzo, madhara na namna ya kukabiliana na mabadiliko hayo.
Aidha, mafunzo hayo yameenda sambamba na kufundishwa namna ya kuandaa mpango mkakati wa kutekeleza na kutathimini shughuli za kimazingira zitakazosaidia kudhibiti mabadaliko ya tabianchi, ikiwa ni pamoja na kupanda miti katika maeneo ya shule, pamoja na kuhamasisha wanafunzi kupanda miti katika makazi yao.
Mafunzo hayo yamehitimishwa kwa walimu kuweka maazimio yatakayowezesha kutekeleza, kusimamia na kufanya tathimini kuhusu shughuli za kutunza mazingira ili kudhibiti mabadiliko ya tabianchi.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.