Jumuiya ya Tawala za Mikoa (ALAT) Mkoa wa Dodoma ikiongozwa na Mwenyekiti wake, Mhe. Almwoni Chaula imeridhishwa na ubora wa miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino.
Hayo yamebainishwa leo, Februari 21, 2026 wakati wa ziara ya ALAT ambapo imetembelea miradi ya afya, Elimu na pamoja na kikundi cha wajasiriamali wanaondesha mradi wa kuku baada ya kupata mkopo wa asilimia kumi kutoka Halmashauri.
Katika ziara hiyo, uongozi na wajumbe wameipongeza Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino kwa kutekeleza miradi mingi ya huduma muhimu za kijamii ili kuhakikisha kuwa wananchi wanapata huduma bora karibu na makazi yao, na imetaka Halmasahuri nyingine za Mkoa wa Dodoma kujifunza kutoka Chamwino.
Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino
Sanduku la posta: 1126 Dodoma
Simu ya Mezani: 026 296 1511
Simu ya Mkononi:
Barua Pepe: ded@chamwinodc.go.tz
Hakimiliki©2017 Halmashauri ya Wilaya ya Chamwino. Haki zote Zimehifadhiwa.